-
Baraza la Usalama la UN lapasisha azimio la kusimamisha vita Gaza haraka iwezekanavyo
Mar 26, 2024 04:27Azimio la kusimamisha vita huko Ukanda wa Gaza hatimaye limepasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya miezi kadhaa ya mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo hilo.
-
Guterres: Nimefunga Swaumu ya Ramadhani kuheshimu imani ya Waislamu wa Gaza
Mar 26, 2024 00:55Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amefichua kwamba alifunga Swaumu ya Ramadhani wakati wa safari yake ya mshikamano na watu wa Gaza ili kuonyesha heshima kwa imani za Waislamu aliowatembelea, akimaanisha ziara yake ya kutembelea kivuko cha Rafah siku ya Jumamosi na ziara yake mjini Cairo Jumapili wiki hii.
-
Russia yatilia shaka madai ya kuhusika Daesh katika shambulizi la kigaidi la Moscow
Mar 25, 2024 23:23Russia imetilia shaka madai ya Marekani kwamba kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limehusika na shambulio kwenye ukumbi wa tamasha nje ya jiji la Moscow, ambalo liliua watu 137, huku mahakama ya Moscow ikiwafungulia mashtaka wahusika wa shambulio hilo ambao walikamatwa kwa tuhuma za ugaidi.
-
Undumakuwili wa Marekani kuhusiana na utawala wa Kizayuni na vita vya Gaza
Mar 25, 2024 22:39Marekani, ikiwa ni mshirika muhimu zaidi na muungaji mkono asiye na masharti wa utawala wa Kizayuni wa Israel, inatekeleza sera ya undumakuwili kuhusu utawala huo na jinai zake. Kwa upande mmoja, katika kitendo cha kuonyesha mshikamano na Israel, Washington imetangaza msaada mpya wa kijeshi kwa utawala huo sambamba na kukata misaada kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Wapalestina UNRWA.
-
Guterres akiri kashfa ya kimaadili ya utawala wa Kizayuni katika kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Mar 25, 2024 22:30Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametembelea kivuko cha Rafah (kati ya Ukanda wa Gaza na Misri), katika mwezi wa sita wa mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni huko Gaza, na kukitaja kitendo cha utawala huo wa Kizayuni cha kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kuwa ni "kashfa ya kimaadili".
-
Mkutano wa Umoja wa Mabunge unaendelea Geneva kwa kuhudhuriwa na Iran
Mar 25, 2024 08:31Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani, kama chombo kikubwa zaidi cha utungaji sheria chenye nchi wanachama zaidi ya 180, ukiwemo ujumbe kutoka Iran unafanyika mjini Geneva Uswisi kwa kauli mbiu ya "Diplomasia ya Bunge, Ujenzi wa Daraja la Amani na Maelewano".
-
Kijana, Islam, aliyeokoa watu zaidi 100 katika hujuma ya kigaidi ya Moscow apewa nishani ya ushujaa
Mar 24, 2024 22:42Kijana Muislamu mwenye umri wa miaka 15 aliyeokoa zaidi ya watu mia moja wakati wa hujuma ya kigaidi kwenye ukumbi wa tamasha wa Crocus City Hall nje kidogo ya jiji la Moscow, siku ya Ijumaa iliyopita, ametunukiwa nishani ya ushujaa.
-
Matteo Salvini: Macron mpiga ngoma ya vita ni "hatari" kwa Ulaya
Mar 24, 2024 22:41Naibu Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Salvini, amesema Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ni "mchochezi wa vita" na ni "hatari" kwa Ulaya kwa kuendelea kushikamana na msimamo wake wa kutuma wanajeshi wa nchi kavu wa nchi za Magharibi huko Ukraine.
-
Ugaidi, changamoto ya pamoja ya kieneo na wajibu wa kuwa macho
Mar 24, 2024 09:14Katika kipindi cha chini ya wiki moja kumetokea miripuko miwili na shambulio kubwa la kigaidi na la umwagaji damu huko Kandahar Afghanistan na kwenye viunga vya mji mkuu wa Russia, Moscow.
-
Idadi ya waliofariki katika shambulio la Moscow yapindukia 130, ISIS-K yadai kuhusika
Mar 24, 2024 03:06Vyombo vya sheria na usalama vya Russia vimesema idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kigaidi la siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa tamasha la muziki wa Crocus City Hall nje kidogo ya jiji la Moscow imepindukia watu 130.