-
UN yashtushwa na mashambulizi mabaya ya anga ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya
Mar 19, 2024 23:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres "amesikitishwa" na ripoti za mashambulizi ya anga yanayoendelea nchini Myanmar ambayo yameua zaidi ya raia 20 katika kitongoji cha Minbya katika jimbo lenye Waislamu wengi la Rakhine siku ya Jumatatu.
-
Mwaka 2023 ulivunja rekodi zote za joto duniani
Mar 19, 2024 23:09Mwaka 2023 ulikuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika rekodi zote zilizowahi kunukuliwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO katika ripoti yake iliyotolewa Jumanne huko Geneva, Uswisi.
-
WHO: Oparesheni za kijeshi dhidi ya Rafah zitasababisha maafa halisi
Mar 19, 2024 08:24Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitahadharisha Israel kuhusu oparesheni yoyote ya kijeshi katika mji wa Rafah na kusema, misaada ambayo imewasili Ukanda wa Gaza haitoshi kukidhi mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.
-
BBC kuchunguza matumizi ya mitandao ya kijamii ya wafanyakazi wake baada ya ripota 'kuunga mkono' ujumbe dhidi ya Israel
Mar 19, 2024 05:55Shirika la Utangazaji la Serikali ya Uingereza, BBC litachunguza matumizi ya mitandao ya kijamii baada ya mwandishi wake "kuunga mkono" jumbe zinazoilaumu Israel kama utawala wa "mauaji ya kimbari" na kuunga mkono haki ya Wapalestina kupinga uvamizi wa Israel.
-
Forensic Architecture yaishutumu Israel kwa "kufanya mauaji ya kimbari" huko Gaza
Mar 19, 2024 04:28Shirika la Forensic Architecture limesema kuwa Israel inatekeleza "ugaidi wa kijiografia" ili kupanua operesheni ya kuwahamisha wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa mabavu, likibainisha kuwa hatua hizi zinaonyesha mwelekeo wa kufanya uhalifu wa mauaji ya kimbari.
-
Ushindi mkubwa wa Putin katika uchaguzi wa rais wa Russia
Mar 19, 2024 02:42Tume Kuu ya Uchaguzi ya Shirikisho la Russia imetangaza kuwa Vladimir Putin, rais wa sasa wa nchi hiyo, ameshinda uchaguzi wa karibuni kwa asilimia 87.32 ya kura na hivyo kupata fursa nyingine ya kuwa rais wa Russia kwa muhula mwingine wa miaka sita. Kwa mujibu wa tangazo la tume hiyo, kiwango cha ushiriki katika uchaguzi kilikuwa cha zaidi ya asilimia 70.
-
Borrell: Gaza limegeuka kaburi kubwa zaidi la wazi duniani
Mar 18, 2024 23:59Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya huku akieleza wasiwasi mkubwa alionao kuhusu mgogoro wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza amesema kuwa, eneo hilo la Wapalestina lililozingirwa limegeuka na kuwa kaburi kubwa zaidi la wazi duniani.
-
Wanafunzi wa kigeni washambuliwa India kwa kusali Tarawehe kwenye dakhalia ya chuo
Mar 18, 2024 07:42Wanafunzi wasiopungua wanne wa kigeni wamejeruhiwa baada ya kundi la Wahindu wenye chuki za kidini kuvamia dakhalia ya chuo kikuu katika jimbo la Gujarat magharibi mwa India na kushambulia kundi la wanafunzi waliokuwa wanasali Sala ya Tarawehe katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
-
Putin ashinda uchaguzi wa rais wa Russia kwa kishindo, apata takriban asilimia 88 ya kura
Mar 18, 2024 02:00Huku kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais wa Russia kukiwa kunaendelea, matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Vladimir Putin ameshinda kwa kishindo kwa kupata takriban asilimia 88 ya kura zote za kuwania muhula mwingine wa miaka sita madarakani.
-
Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yaendelea kushuhudiwa katika nchi mbalimbali
Mar 17, 2024 23:33Wananchi katika nchi mbalimbali kwa mara nyingine tena wamefanya maandamano na mikusanyiko mbalimbali katika kuwaunga mkono na kuonyesha mshikamano kwa raia madhulumu wa Palestina.