Mar 19, 2024 06:12 UTC
  • Ushindi mkubwa wa Putin katika uchaguzi wa rais wa Russia

Tume Kuu ya Uchaguzi ya Shirikisho la Russia imetangaza kuwa Vladimir Putin, rais wa sasa wa nchi hiyo, ameshinda uchaguzi wa karibuni kwa asilimia 87.32 ya kura na hivyo kupata fursa nyingine ya kuwa rais wa Russia kwa muhula mwingine wa miaka sita. Kwa mujibu wa tangazo la tume hiyo, kiwango cha ushiriki katika uchaguzi kilikuwa cha zaidi ya asilimia 70.

Vladislav Davankov mwenye umri wa miaka 40, wa Chama Kipya cha Watu, Leonid Slutsky mwenye umri wa miaka 56, mkuu wa Chama cha Dmokrasia ya Kileberali cha Russia na Nikolai Kharitonov mwenye umri wa miaka 75 wa Chama cha Kikomunisti cha Russia, ni wapinzani wakuu waliochuana na Putin katika uchaguzi huo. Kila mmoja wa wagombea hao watatu alishinda kati ya asilimia 3 hadi 4 ya kura.

Mnamo 2000, Putin alikuwa rais wa Shirikisho la Russia kwa mara ya kwanza ambapo aliongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka minne. Kisha akachaguliwa tena mwaka 2004 na kushikilia wadhifa huo hadi 2008. Baada ya hapo, amekuwa rais wa Russia tangu 2012 hadi sasa. Kufuatia ushindi wake wa karibuni, Putin sasa atakuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka mingine 6.

Baada ya kushinda, amewaambia waandishi wa habari kwamba matokeo ya uchaguzi huu yataiwezesha jamii ya Russia kuungana na kuwa na nguvu zaidi. Amesisitiza kuwa maandamano yaliyofanywa dhidi yake na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Alexei Navalnym aliyeaga dunia karibuni, hayakuwa na taathira yoyote katika matokeo ya uchaguzi.

Rais Vladimir Putin wa Russia

Putin amesema licha ya madai mengi yanayotolewa, lakini hakuna demokrasia katika nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani na kwamba mfumo wa uchaguzi nchini Russia una uwazi zaidi kuliko wa Marekani. Wafuasi wa Alexei Navalny wamedai kuwa idadi ya kura zilizotangazwa kwa manufaa ya Vladimir Putin si ya kweli. Kwa upande mwingine, Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, akiashiria ushiriki mkubwa wa wapiga kura katika balozi za Russia nje ya nchi, amesema kwamba walifika katika balozi hizo kwa ajili ya kunufaika na fursa waliyoandaliwa na nchi yao, Russia, licha ya vitisho vingi vinavyotolewa dhidi ya nchi hiyo na madola ya Magharibi.

Ushindi wa Vladimir Putin katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu ni wa kuzingatiwa sana kwa kutilia maanani kiwango kikubwa cha ushiriki wa wananchi. Katika uchaguzi wa rais mwaka 2018, Putin alishinda kwa asilimia 76 ya kura. Kwa msingi huo, ni wazi kwamba kiwango hicho cha ushiriki kimevunja rekodi na ni aina fulani ya kura ya maoni kwa manufaa ya Putin. Sasa, miaka sita baadaye, na katika mwaka wa tatu wa vita vya Ukraine ambapo nchi za Magharibi zimeiwekea Russia vikwazo vikubwa na kuendesha propaganda chafu dhidi ya Putin, rais huyo kuibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia 87 ya kura ni ishara ya wazi kuwa propaganda za Magharibi dhidi yake sio tu hazikuzaa matunda, bali imani ya watu wa Russia kwake imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Adui mkuu wa Russia, yaani Marekani, kabla ya kufanyika uchaguzi wa karibuni, ilifanya uingiliaji mkubwa dhidi ya Moscow na vita vya propaganda dhidi ya Vladimir Putin kupitia vyombo vya habari kwa lengo la kuvuruga mchakato wa uchaguzi na kuchafua jina lake kati ya watu wa Russia, lakini sasa kura za Warussia kwa Putin zimethibitisha wazi kuwa hatua hizo za uadui hazikufua dafu.

Ni wazi kwamba kuendelea uongozi wa Vladimir Putin kama rais wa Russia kumekuwa na nafasi muhimu katika maendeleo ya nchi hiyo katika miongo miwili iliyopita, na kwa kuzingatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu na kuendelea uongozi wake hadi kwa uchache 2030, inatarajiwa kwamba atakuwa na jukumu muhimu katika ustawi zaidi wa nchi hiyo kubwa zaidi ulimwenguni.

Uchochezi wa Marekani katika vita vya Ukraine dhidi ya Russia

Kwa kuzingatia kuendelea vita vya Ukraine na vikwazo vikubwa na visivyo na mfano wake vya Magharibi dhidi ya Russia, Putin ameweza kudhibiti matatizo ya nchi hiyo kwa kiasi kikubwa. Licha ya ukweli kwamba Russia inakabiliwa na matatizo yanayosababishwa na uhaba wa nguvu kazi, mfumuko wa bei na viwango vya juu vya riba, lakini mafanikio ya Moscow ya kutosalimu amri mbele ya taathira za bei iliyoainishwa na nchi za Magharibi kwa mafuta ya Russia na upanuzi wa kiuchumi na kibiashara katika uhusiano wake na nchi za Mashariki, ni baadhi ya mambo ambayo yamechangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Hii ni pamoja na kuwa Russia imeweza kulinda nafasi yake ya kijeshi katika vita na Ukraine ambapo inaendelea kuimarisha nafasi yake katika ardhi zilizojitangazia uhuru ma kujitenga na Ukraine. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba ameweza kupata mafanikio na matokeo muhimu katika mgogoro na mvutano wake mkubwa na nchi za Magharibi, zikiongozwa na Marekani.

Tags