-
Afisa wa Umoja wa Mataifa: Hali bado ni mbaya huko Gaza
Nov 25, 2025 04:00Ramiz Alakbarov, Naibu Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa Mchakato wa Amani wa Mashariki ya Kati, ameonya kwamba hali katika Ukanda wa Gaza "inaendelea kuwa mbaya," na kusema kuwa familia nyingi haziwezi kumudu kununua kuku na nyama licha ya upatikanaji wa bidhaa za msingi za chakula na kuboreshwa kwa bei za bidhaa hizo.
-
Umoja wa Mataifa: Mwanamke mmoja huuliwa kila baada ya dakika 10
Nov 25, 2025 03:08Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana Jumatatu ilisema kwamba karibu wanawake 50,000 waliuawa na jamaa zao mwaka wa 2024, kwa kiwango cha mwanamke mmoja kila baada ya dakika 10, na kuelezea masikitiko yake kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana katika kupambana na mauaji ya wanawake.
-
Kura ya maoni: Wamarekani wengi wanapinga hatua za kijeshi dhidi ya Venezuela
Nov 24, 2025 23:14Kura ya maoni iliyofanywa na CBS News ikishirikiana na kampuni ya utafiti ya YouGov imeonyesha kuwa Wamarekani wengi wanapinga hatua zozote za kijeshi dhidi ya Venezuela.
-
Rais wa Korea Kusini: Mifumo ya kimataifa ya AI inapasa kuhakikisha mataifa yote yanapa teknolojia hiyo kwa usawa
Nov 24, 2025 23:10Rais wa Korea Kusini, Lee Jae Myung amesema kuwa mifumo ya kimataifa ya akili mnemba (AI) inapasa kuhakikisha kuwa mataiafa yote yanapata teknolojia hiyo kwa usawa.
-
Kwa nini Macron anaamini kuwa G20 inakaribia kuporomoka?
Nov 24, 2025 04:24Katika ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20 mjini Johannesburg, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema katika hotuba isiyo ya kawaida kuwa kundi hilo limepoteza uwezo wake wa kutatua migogoro ya kimataifa.
-
Kumbukumbu ya Uhalifu wa Magharibi - Wounded Knee Massacre; Mauaji ya Wahindi Wekundu huko South Dakota, 1890
Nov 23, 2025 23:49Mauaji makubwa ya Wounded Knee Massacre hapo 1890 huko South Dakota, Marekani, yalikuwa mojawapo ya ukatili wa umwagaji damu mkubwa zaidi dhidi ya Wahindi Wekundu katika historia ya Marekani, ambayo yalisababisha mauaji ya mamia ya watu wa jamii ya Lakota na kukomesha mapambano yao makubwa katika karne ya 19.
-
Sera za vikwazo dhidi ya Cuba: Mfano wa mbinu ya mabavu ya Washington katika kuamiliana na nchi nyingine
Nov 23, 2025 10:46Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa vikwazo vya Marekani vimeifanya hali ya kibinadamu nchini Cuba kuwa mbaya sana na ametaka kuondolewa haraka vikwazo hivyo.
-
Venezuela: Tutatoa jibu kali kwa uvamizi wowote wa Marekani dhidi yetu
Nov 23, 2025 08:35Waziri wa Ulinzi wa Venezuela amesema kuwa, nchi yake imesimama kidete dhidi ya vitisho vyote vya hivi karibuni vya kijeshi vya Marekani.
-
Ripoti: Hujuma dhidi ya Misikiti Uholanzi zimeongezeka
Nov 23, 2025 08:35Ripoti mpya imeonesha kuwa matukio ya vurugu na hujuma dhidi ya misikiti nchini Uholanzi yameongezeka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa mtandao wa misikiti K9.
-
Marekani yabatilisha viza ya waziri wa zamani wa Afrika Kusini aliyefanikisha kesi ya ICJ dhidi ya Israel
Nov 23, 2025 03:31Marekani imefuta viza ya waziri wa zamani wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor mapema wiki hii, katika kile kinachoonekana kama hatua za hivi karibuni za Washington za kuiadhibu Pretoria kwa sababu kuuburuza utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa mauaji ya kimbari uliyofanya dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.