Moto uliochochewa na upepo umeua watu zaidi ya 34 Algeria
(last modified Tue, 25 Jul 2023 14:59:00 GMT )
Jul 25, 2023 14:59 UTC
  • Moto uliochochewa na upepo umeua watu zaidi ya 34 Algeria

Moto wa nyika usiodhibitiwa unaoendelea katika nchi za Algeria na Tunisia huko kaskazini mwa Afrika wakati huu wa wimbi la joto kali umesababisha vifo vya makumi vya watu na kuwalazimisha maelfu ya wengine kuyahama makazi yao.

 Watu zaidi ya 34 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Algeria wakiwemo wanajeshi kumi katika mkasa huo wa moto ulioyaathiri maeneo ya makazi ya raia. 

mashuhuda wanasema: "Moto huo ulianza katika eneo la Grouma na kuenea katika eneo la Beni Malah na mwishowe ukaingia katika eneo la Bourebach na kuchoma moto kila kitu. Baadhi ya watu wamepoteza kila kitu." 

Algeria na maafa ya moto wa msituni 

Algeria inayopatikana kaskazini mwa Afrika imesajili matukio ya 97 ya moto katika mikoa 16 yaliochochewa na upepo mkali  huku joto likifia nyuzijoto 48 katika baadhi ya maeneo ya Algeria. 

Maeneo yaliyoathiriwa sana na moto huo uliochochewa na upepo mkali ni Bejaia na Jijel huko mashariki mwa mji mkuu, Algiers. Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ametoa mkono wa pole na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wanajeshi na raia wa kawaida waliopoteza maisha katika mkasa wa moto.