Congo yaazimia kupambana na homa ya manjano
(last modified Tue, 28 Jun 2016 14:10:19 GMT )
Jun 28, 2016 14:10 UTC
  • Congo yaazimia kupambana na homa ya manjano

Waziri wa Afya wa Congo ametangaza azma ya nchi yake ya kupambana na kasi ya maambukizi ya homa ya manjano.

Dr Félix Kabange Numbi Mukwampa amesema kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapambana ipasavyo na ugonjwa huo na kwamba unaweza kudhibitiwa.

Waziri Kabange ameongeza kuwa, operesheni ya kutoa chanzo ya homa ya manjano kwa raia karibu milioni 12 nchini humo imeanza na itaendelea kwa kasi kubwa.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani (WHO) siku chache zilizopita lilieleza wasiwasi wake kuhusu maambukizi ya ugonjwa hatari wa homa ya manjano kutoka Angola hadi maeneo mengine ya dunia na kuwataka wanaosafiri nchini humo kupata chanjo ya homa hiyo.

Watu wasiopungua 258 wamefariki dunia hadi sasa kutokana na homa ya manjano tangu ugonjwa huo ulipuke nchini Angola mwaka 2015.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa homa ya manjano vinatokea katika bara la Afrika.