Mar 22, 2024 06:38 UTC
  • Abdelmajid Tebboune
    Abdelmajid Tebboune

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria imeeleza kuwa nchi hiyo itaitisha uchaguzi wa mapema wa rais mwezi Septemba mwaka huu, miezi mitatu kabla ya muda uliokuwa umepangwa hapo awali.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais wa Algeria imeeleza kuwa, imeamuliwa kufanya uchaguzi wa mapema wa urais tarehe 7 Septemba mwaka huu kufuatia mkutano ulioongozwa na Rais wa nchi hiyo Abdelmadjid Tebboune na kuhudhuriwa na wabunge na mkuu wa majeshi.

Rais Tebboune ambaye atatimiza miaka 79 ifikapo mwezi Novemba, alichaguliwa kushika hatamu za uongozi mwezi Disemba mwaka 2019 baada ya maandamano ya waungaji mkono wa demokrasia mwezi Februari mwaka huo ambayo yalimlazimisha Rais aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu huko Algeria, Abdelaziz Bouteflika, kujiuzulu.

Rais wa Algeria aliyejiuzulu, Abdelaziz Bouteflika 

Rais wa sasa wa Algeia Abdelmajid Tebboune ambaye muhula wake wa uongozi wa miaka mitano ulipasa kumalizika mwezi Disemba mwaka huu mwaka 2019 alishinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 58 ya kura. 

Tebboune hajasema iwapo atawania muhula wa pili madarakani na hakukuwa na maelezo ya moja kwa moja kwa nini uchaguzi wa mapema wa urais umeitishwa.

Tags