Mtandao wa magidi wasambaratishwa A. Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11071-mtandao_wa_magidi_wasambaratishwa_a._kusini
Vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini vimetangaza kuwa vimefanikiwa kuwatia nguvuni washukiwa wanne wa ugaidi katika operesheni maalumu iliyofanywa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 12, 2016 03:45 UTC
  • Mtandao wa magidi wasambaratishwa A. Kusini

Vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini vimetangaza kuwa vimefanikiwa kuwatia nguvuni washukiwa wanne wa ugaidi katika operesheni maalumu iliyofanywa nchini humo.

Luteni Jenerali Mthandazo Ntlemeza ambaye ni afisa wa ngazi za juu wa vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini amesema kuwa, waliotiwa nguvuni wana umri wa kati ya miaka 20 na 24 na kwamba mwaka jana walitaka kwenda kujiunga na makundi ya kigaidi nchini Syria.

Luteni Jenerali Ntlemeza ameongeza kuwa, katika operesheni hiyo vyombo vya usalama vimekamata zana za mawasiliano na vifaa vingine vinavyotumiwa na magaidi. Afisa huyo wa ngazi za juu amesisitiza kuwa juhudi za kuwatia nguvuni wanachama wengine wa mtandao huo wa kigaidi zinaendelea.

Afisa huyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuripoti matukio na hatakati zote zinazotia shaka.