Jun 01, 2024 07:49 UTC
  • Libya yajiunga kwenye kesi ya nchi kadhaa dhidi ya utawala wa Kizayuni

Mwakilishi wa Libya katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) amesema kuwa; mahakama hiyo Umoja wa Mataifa (UN) imekubali ombi la Tripoli la kujiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Ahmad Al Jahani  mwakilishi wa Libya katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki  amesema hayo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki imekubali ombi la Libya la kujiunga na kesi ya malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Amesema kuwa Inatarajiwa kwamba hoja iliyoandikwa ya Libya kuhusu kesi hii itawasilishwa kikamilifu mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) tarehe 10 Julai.

Shukrani za Hamas kwa kujiunga Libya katika kuulalamikia utawala wa Kizayuni

Kabla ya hapo Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ilikuwa imetangaza kuwa Mexico nayo imeomba kujiunga na malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) imetangaza katika taarifa yake kwamba Mexico inataka kujiunga na kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni kuhusu kukiuka makubaliano ya kuharamishwa jinai ya mauaji ya halaiki.

Mexico imewasilisha ombi hilo ikinukuu kifungu cha 63 cha Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambacho kinazipa nchi nyingine haki ya kuingilia kati kutoa maoni na kutafsiri makubaliano yaliyotajwa hapo juu.

Mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana 2023, Afrika Kusini iliwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu dhidi ya utawala wa Kizayuni kutokana na utawala huo kukiuka makubaliano ya kupigwa marufuku jinai za mauaji ya halaiki.

Baada ya hapo, nchi kadhaa zikiwemo Mexico, Uturuki, Colombia, Nicaragua na Libya ziliomba kujiunga na kesi hiyo kwa ajili ya kuwatetea na kuwaunga mkono Wapalestina wa ukanda wa Gaza wanaouawa kila siku na utawala haramu wa Israel.

Tags