Jun 28, 2024 03:52 UTC
  • Watu  755,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Sudan

Wataalamu na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa, mapigano yanayoendelea nchini Sudan baina ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF yatapelekea watu 755,000 kuwajihiwa na baa la njaa na uhaba mkubwa wa chakula katika miezi michache ijayo.

Wataalamu hao wa UN wamesema, makabiliano baina ya wapiganaji wa RSF wanaoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo na askari wa jeshi la Sudan linaloongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, yameipelekea nchi hiyo ikumbwe na mgogoro mkubwa wa njaa, ambao haujawahi kushuhudiwa tangu ule mgogoro wa Darfur wa miaka ya 2000.

Ripopti ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa imesema, Wasudan zaidi ya milioni 8.5 wanabakbiliwa na ubaha wa chakula, na kwamba 755,000 miongoni mwao wapo katika hatari ya kufa njaa ndani ya miezi michache ijayo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.

Imesema maeneo ambayo wakazi wake wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya baa la njaa katika nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika ni Khartoum; maeneo ya Darfur na Kordofan, na mikoa ya Blue Nile na al-Jazira. 

Njaa Sudan

Tangu katikati ya Aprili 2023, jeshi la Sudan, likiongozwa na al-Burhan, na vikosi vya RSF vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo, vimekuwa vikipigana, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 15,000.

Aidha kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, takriban Wasudani milioni 8.5 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita hivyo.

Tags