Udhalilishaji wa kingono watumiwa kama silaha ya vita katika mzozo huko Sudan
Pande husika katika vita vya ndani nchini Sudan zimetekeleza udhalilishaji wa kingono na vitendo vingine vya unyanyasaji kama silaha ya vita tangu kuanza mapigano ya ndani nchini humo mwezi Aprili mwaka jana.
Mona Rishmawi Mjumbe wa Tume Huru ya Kimataifa ya Kutafuta Ukweli ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan ametoa maoni yake kuhusu ripoti za udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake huko Sudan.
Amesema kuwa kufuatia mzozo unaoendelea huko Sudan, wanawake wengi wamekuwa wakimbizi, na idadi kubwa ya wengine pia wamelazimika kusafiri hadi nchi nyingine peke yao kwa sababu waume zao wameuawa.
"Wanawake wa Sudan mara kwa mara wamekuwa wakitangatanga na kukabiliwa na hatari mbalimbali wakati wa safari zao wakitafuta hifadhi ikiwemo kukabiliwa na udhalilishaji wa kingono na vitendo vingine vya ukatili," amesema mjumbe huyo wa Tume Huru ya Kimataifa ya Kutafuta Ukweli ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan, Mona Rishmawi."
Ameongeza kuwa, vitendo vya udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake vimeenea pakubwa katika maeneo ya vita na mizozo.