Wapiganaji wa RSF washambulia kijiji na kuua watu 42 katikati mwa Sudan
(last modified Thu, 21 Nov 2024 07:47:22 GMT )
Nov 21, 2024 07:47 UTC
  • Wapiganaji wa RSF washambulia kijiji na kuua watu 42 katikati mwa Sudan

Watu wasiopungua 42 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika kijiji cha Wad Oshaib katika jimbo la kati la al Jazira nchini Sudan.

Kundi la wanaharakati kwa jina la "The al Jazira Conference" limetoa taarifa likiwatuhumu wapiganaji wa RSF kwa kukiuka pakubwa haki za binadamu na kutekeleza mauaji makubwa ya raia. 

RSF ilitekeleza mauaji hayo kwa risasi usiku wa kuamkia juzi na jana asubuhi huku wengine 27 wakiaga dunia kwa kuzingirwa na kukosa msaada wa tiba. 

Juzi Jumanne wanaharakati nchini Sudan waliripoti kuwa watu 27 wameuawa kutokana na kuenea magonjwa ya mlipuko na uhaba wa dawa za matibabu na chakula vilivyosababishwa na mzingiro wa RSF.  

Mapigano kati ya RSF na Wanajeshi wa Sudan yalianza tena huko Al-Jazira  Oktoba 20 baada ya Abu Aqla Kikil, Kamanda wa wanamgambo wa RSF katika jimbo hilo, kuasi na kutangaza utiifu wake kwa jeshi.

Kamanda, Abu Aqla Kikil aliyejiunga na jeshi la Sudan