Hizbullah yaonesha nguvu zake, yaporomosha ndogo za maadui
(last modified Sun, 01 Jun 2025 02:21:55 GMT )
Jun 01, 2025 02:21 UTC
  • Hizbullah yaonesha nguvu zake, yaporomosha ndogo za maadui

Licha ya Marekani kusimamia yenye vita kuusaidia utawala wa Kizayuni, na licha ya maadui hao kuwa na ndoto kwamba huenda Hizbullah ya Lebanon ikapoteza nguvu zake, lakini maadui hao wamejikuta wamo katikati ya vita tata mno ambavyo vinazidi kusambaratisha ndoto zao.

Hayo yamo kwenye makala iliyochapishwa na gazeti la al Akhbar la Lebanon kwa kalamu ya kiuchambuzi ya Haitham Al-Moussawi na kuandika: Vita dhidi ya Lebanon havikuisha kwa tangazo la usitishaji vita la Novemba 27, 2024. Bali, viliingia katika awamu mpya kwa kasi na kwa mbinu tofauti kiasi kwamba, licha ya makamanda na viongozi wa ngazi za juu wa Hizbullah kuuawa shahidi katika njia ya ukombozi wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu Msikiti wa al Aqsa na Quds, lakini maadui wameshindwa kufikia malengo yao ya kimkakati.

Mwandishi wa makala hiyo amefichua pia wasiwasi mkubwa unaozitesa roho za viongozi wa Marekani na Israel kuhusu kuendelea kuwa na nguvu harakati ya Hizbullah. Makala hiyo imemnukuu Eyal Zamir, Mkuu wa Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel alikiri hivi karibuni katika kikao kilichohudhuriwa na makamanda mbalimbali wa jeshi la Israel akiwemo Meja Jenerali Uri Gordin na maafisa wengine wa kijeshi kwamba "vita dhidi ya Hizbullah bado havijaisha." 

Baada ya kuanguka utawala wa Rais Bashar al-Assad, serikali mpya ya Syria haifichi nia yake ya kujipendekeza kwa nchi za Magharibi na kupigia magoti malengo ya madola hayo ya kibeberu katika eneo hili, hususan kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni. 

Lakini jambo jingine muhimu katika matukio ya kieneo baada ya vita vya Lebanon ni kuibuka nguvu mpya ya kisiasa ambayo imechukua mkondo wa kupinga Muqawama na mapambano dhidi ya Israel ikitoa mwito wa kupokonywa silaha makundi ya Muqawama, na kupuuza tishio na hatari za utawala wa Israel kwa maisha ya hivi sasa na ya baadaye ya Lebanon na nchi za eneo hili. Lakini yote hayo hayajaizuia Hizbullah ya Lebanon kuzidi kuimarisha nguvu zake.