Malori ya misaada yawasili Sudan baada ya kukwama kwa miezi kadhaa
(last modified 2024-08-22T12:01:37+00:00 )
Aug 22, 2024 12:01 UTC
  • Malori ya misaada yawasili Sudan baada ya kukwama kwa miezi kadhaa

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa zaidi ya malori 12 kutoka mashirika ya misaada yamevuka mpaka na kuingia Sudan kupitia kivuko cha Adre katika mpaka na Chad ili kuleta misaada kwa ajili ya raia walioathiriwa na njaa katika  jimbo la Darfur.

Stephane Dujarric ameeleza kuwa malori hayo yamepakia magunia ya mtama, kunde, mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya watu 13,000 ambao wako katika hatari ya njaa katika eneo la Kereneik la Darfur Magharibi.

Wakazi wa Darfur na tatizo la uhaba wa chakula 

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limepongeza hatua hiyo likisema kuwa misaada muhimu iliyotolewa itasaidia zaidi ya watu 12,000 wenye uhitaji. 

Baraza la uongozi la Sudan Alhamisi iliyopita lilieleza kuwa litaruhusu kutumiwa mpaka wa Adre kwa muda wa miezi mitatu, hatua ambayo ilisubiriwa kwa muda mrefu na mashirika ya misaada ya kibinadamu.

Wakati huop huo, Waangalizi wa Kimataifa wamesema, zaidi ya watu milioni 6 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula katika jimbo la Darfur, ambalo linadhibitiwa na vikosi vya msaada wa haraka (RSF) vinavyopigana dhidi ya jeshi la Sudan. 

 

 

Tags