Iran, Kenya kuimarisha ushirkiano wa kiuchumi
Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran Ali Tayebnia ameelezea matumaini kuwa, baada ya kuondolewa vizingti vya uhusiano wa kibenki, Kenya na Iran zitaweza kuimarisha uhusiano katika sekta za biashara na viwanda.
Tayebnia aliyasema hayo Jumanne mjini Nairobi wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Patrick Ngugi Njoroge Gavana wa Banki Kuu ya Kenya. Wawili hao wamejadli njia za kuimarisha uhusiano wa Tehran na Nairobi.
Gavana wa Banki Kuu ya Kenya amesema kuimarishwa uhusiano wa kiuchumi na Iran ni fursa nzuri kwa Kenya. Ameongeza kuwa: "Tunasubiri kwa hamu kuondolewa vizingiti vya ushirikiano wa kibanki na Iran."
Tayebnia yuko mjini Nairobi, Kenya kushiriki katika ufunguzi wa Kikao cha 14 cha Uwekezaji Duniani cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara (UNCTAD).