UN: Mafuriko nchini Sudan Kusini yaathiri watu milioni 1.4
(last modified Sun, 10 Nov 2024 03:30:15 GMT )
Nov 10, 2024 03:30 UTC
  • UN: Mafuriko nchini Sudan Kusini yaathiri watu milioni 1.4

Mafuriko makubwa nchini Sudan Kusini yameathiri takriban watu milioni 1.4, na kuwakosesha makazi wengine 379,000. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika

OCHA imesema watu milioni 1.4 wameathiriwa na mafuriko katika kaunti 43 huku majimbo ya Jonglei na Bahr el Ghazal Kaskazini yakiwa yanajumuisha zaidi ya asilimia 51 ya watu walioathirika.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa zaidi ya watu 379,000 walikimbia makazi yao katika kaunti 22 na Abyei.

Taarifa hiyo ilisema kuongezeka kwa malaria kumeripotiwa katika majimbo ya Jonglei, Unity, Upper Nile, Kaskazini mwa Bahr el Ghazal, Equatoria ya Kati, na  Equatoria Magharibi, na hivyo kuulemea mfumo wa afya na kuzidisha hali mbaya katika nchi hiyo.

Mvua kubwa na mafuriko Sudan Kusini mwaka hii ni mojawapo ya mvua mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa nchini humo.