Maporomoko ya udongo yauwa 12 nchini Cameroon
(last modified Mon, 11 Nov 2024 02:23:32 GMT )
Nov 11, 2024 02:23 UTC
  • Maporomoko ya udongo yauwa 12 nchini Cameroon

Wafanyakazi wa huduma za uokoaji wamepata miili 12 ya watu waliopoteza maisha katika maporomoko ya udongo yaliyomeza barabara huko magharibi mwa Cameroon.

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imeripoti kuwa mbali na kupoteza maisha watu 12, makumi ya watu wengine hawajulikani walipo hadi sasa huko magharibi mwa Cameroon. 

Maporomoko mawili ya ardhi yaliiathiri barabara ya Dschang cliff wiki hii ambapo magari kadhaa yaliyokuwa yamepakia abiria yaliathirika. 

Barabara za Cameroon ni hatari sana, na karibu vifo 3,000 hutokea nchini humo kila mwaka kwa ajali. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za karibuni za Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mapema mwezi Septemba mwaka huu lori lililokuwa limebeba abiria lilitumbukia katika barabara ya miamba kwenye bonde karibu na mji wa Dschang na kuuwa watu 4 na kujeruhi 62 wakiwemo watoto 8.