Amnesty International: Silaha za Ufaransa zinatumika vitani Sudan licha ya vikwazo
(last modified Thu, 14 Nov 2024 11:10:58 GMT )
Nov 14, 2024 11:10 UTC
  • Amnesty International: Silaha za Ufaransa zinatumika vitani Sudan licha ya vikwazo

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetangaza kuwa, silaha za Ufaransa zimekuwa zikitumika katika vita vya wenyewe kkwa wenyewe nchini Sudan licha ya vikwazo vya silaha vyya Umoja wa Mataifa.

Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International ameziambia duru za habari: "Utafiti wetu unaonesha kuwa silaha zilizoundwa na kutengenezwa nchini Ufaransa zinatumika kikamilifu katika uwanja wa vita nchini Sudan" .

Taariofa zaidi zinasema kuwa, teknolojia ya kijeshi ya Ufaransa inatumiwa katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kinyume na vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa.

Inasema wanamgambo wa RSF wanatumia magari katika eneo la Darfur yanayotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo yana vifaa vya Ufaransa wakati wanapambana na jeshi.

Mfumo wa ulinzi wa Galix, uliotengenezwa nchini Ufaransa na makampuni ya KNDS na Lacroix, unatumika kwa vikosi vya nchi kavu kusaidia kukabiliana na mashambulizi ya karibu.

Sudan ilitumbulia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 15 mwaka jana (2023), kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Abdel Fattah al-Barhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo.