Silaha za biolojia za Marekani barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120676-silaha_za_biolojia_za_marekani_barani_afrika
 Wizara ya Ulinzi ya Russia imefichua nyaraka zinazoonyesha kuwa Marekani imeongeza shughuli zake za silaha za kibiolojia katika bara la Afrika.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 27, 2024 07:38 UTC
  • Silaha za biolojia za Marekani barani Afrika

 Wizara ya Ulinzi ya Russia imefichua nyaraka zinazoonyesha kuwa Marekani imeongeza shughuli zake za silaha za kibiolojia katika bara la Afrika.

Naibu Mkuu wa Idara ya Ulinzi ya Russia inayohusika na ulinzi wa Biolojia, Kemikali na Mionzi amefichua kuwa, baada ya kusimamishwa shughuli za Marekani za kimaabara za silaha za biolojia nchini Ukraine, Washington sasa imehamishia shughuli zake hizo katika nchi za Afrika.

Meja Jenerali Aleksey Rtishchev amebainisha kuwa, Marekani imehamishia vitengo kadhaa vya kituo chake cha masuala ya tiba cha Jeshi la Wanamaji katika nchi za Djibouti na Ghana.

Kwa mujibu wa Rtishchev, Washington ina wasiwasi hasa kuhusu juhudi zinazofanywa na Russia na China kushirikiana na mataifa ya Afrika katika kufichua sura halisi ya mipango ya kibiolojia ya kijeshi ya Marekani.

Hii si mara ya kwanza kutangazwa ripoti kuhusu shughuli za vita vya kibiolojia vya Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia, ikiwa ni pamoja na Afrika na hata Asia Mashariki, katika miongo mitatu iliyopita. Kuibuka Ugonjwa Mkali wa Mfumo wa Upumuaji (SARS) nchini China na kisha kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19 katika nchi hiyo, ambao asili yake bado haijafahamika, kumetathmihniwa na weledi wa mambo kama shughuli za vita vya kibiolojia vya Marekani dhidi ya washindani wake.

Katika bara la Afrika pia, majaribio haya ya Marekani yanaendelea kwa uzito zaidi, lakini kutokana ubeberu wa kimataifa kuhodhi vyombo vingi vya habari, taarifa nyingi za uhalifu wa kibiolojia wa Marekani barani  Afrika ama hazichapishwi au zinafanywa kuwa magonjwa ya kawaida na kutangazwa kutumwa vikosi vya misaada katika bara hilo kunahesabiwa kama juhudi za kujaribu kutatua matatizo ya kiafya ya watu wa Afrika.

Meja Jenerali Aleksey Rtishchev,Naibu Mkuu wa Idara ya Ulinzi ya Russia inayohusika na ulinzi wa Biolojia, Kemikali na Mionzi ya Russia

Kwa maneno mengine ni kuwa, inaweza kusemwa kwamba watu wa bara la Afrika daima wamekuwa panya wa maabara ya kibiolojia ya madola ya Magharibi, hasa Marekani.

Kwa hiyo, kulingana na ufichuzi wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Kituo cha Matibabu cha Jeshi la Marekani nchini Kenya kimeweka mtandao wa kufuatilia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza katika Ukanda wa Tropiki Afrika. Nchini Nigeria, kituo cha pamoja cha utafiti wa matibabu na maabara ya matibabu ya kijeshi vimeanzishwa mwaka huu, ambapo wataalamu 10 kutoka Idara ya Ulinzi ya Marekani wapo nchini humo kwa sura ya  kudumu.

Ukweli wa mambo ni kwamba, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inatumia miundombinu na uwezo wa nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na rasilimali watu, kufanya utafiti wake wa kijeshi-kibiolojia.

Kulingana na vyombo vya habari vya Russia , Wakala wa Kupunguza Vitisho vya Ulinzi (DTRA), Shirika la Usalama wa Taifa na Wizara ya Mashauri ya kigeni ya Marekani zinaunga mkono shughuli za maabara za kibiolojia za serikali ya nchi hiyo.

Katika hali hii kama alivyosema Naibu Mkuu wa Idara ya Ulinzi ya Russia inayohusika na ulinzi wa Biolojia, Kemikali na Mionzi ni kuwa, watumiaji wakuu wa utafiti wa kibiolojia wa Pentagon ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza ya Jeshi la Marekani  (USAMRIID) na Kituo cha Taifa cha Tiba cha Kijeshi cha Walter Reed.

 

Alaa kulli haal, ufichuzi wa Wizara ya Ulinzi ya Russia kuhusu kukithiri kwa shughuli za vita vya kibiolojia vya Marekani barani Afrika unaripotiwa katika hali ambayo, hivi karibuni kulichapishwa ripoti zikiwanukuu maafisa wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakitangaza kuenea kwa ugonjwa wa ajabu  na usiojulikana  wenye dalili za mafua. Ugonjwa huo hadi sasa umesababisha vifo vya makumi ya watu katika nchi hiyo. Tanzania pia imewahi kuripoti ugonjwa wa ajabu uliouawa watu kadhaa katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Matukio haya ni ushahidi unaoonyesha kuwa Marekani imeendeleza shughuli zake za utafiti barani Afrika ili kuzalisha kizazi kipya cha silaha hatari za kibiolojia, bara ambalo limekuwa likikandamizwa na nchi za Magharibi hasa Marekani kwa miongo kadhaa, na sasa watu wa bara hilo wanatumika kama panya na viumbe vya kufanyia majaribio katika maabara.