Wanajeshi wa Ufaransa wamefukuzwa kutoka nchi gani za Kiafrika?
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120932-wanajeshi_wa_ufaransa_wamefukuzwa_kutoka_nchi_gani_za_kiafrika
Baada ya Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Senegal serikali ya Ivory Coast pia inataka kuondolewa na kufukuzwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
(last modified 2025-01-03T00:13:23+00:00 )
Jan 03, 2025 00:13 UTC
  • Wanajeshi wa Ufaransa wamefukuzwa kutoka nchi gani za Kiafrika?

Baada ya Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Senegal serikali ya Ivory Coast pia inataka kuondolewa na kufukuzwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Rais wa Ivory Coast alitangaza Jumanne usiku katika hotuba yake mwishoni mwa mwaka uliomalizika hivi karibuni wa 2024 kwa watu wa nchi hiyo kwamba: Kambi ya Kikosi cha 43 cha Wanamaji huko Port Bouet itarejeshwa kwa wanajeshi wa nchi hiyo Januari mwaka huu 2025.

Ufaransa ina kikosi cha wanajeshi 600 nchini Ivory Coast. Kufuatia kushadidi hisia za chuki dhidi ya Ufaransa makoloni ya zamani ya Ufaransa, serikali ya nchi hiyo iliamua kupunguza uwepo wake wa kijeshi katika nchi za Afrika Magharibi na Kati Novemba mwaka jana.

Kuhusiana na hili, idadi ya askari wa Ufaransa ilifikia 600 kutoka askari wapatao 2,200. Hivi sasa idadi hiyo nayo ya wanajeshi wa Ufaransa lazima waondoke Ivory Coast.

Serikali ya Ufaransa ilikuwa ikidhani kwamba kwa kupunguza askari wake, bado itaweza kudumisha ushawishi wake wa kijeshi na kisiasa barani Afrika. Lakini mkakati huu wa Ufaransa pia umeshindwa. Makoloni ya zamani ya Ufaransa yanadai kukomeshwa kabisa kwa utawala wa kisiasa na kiuchumi wa mkoloni huyo wa Ulaya na kutawale anga ya uhusiano wa kuheshimiana na sio msingi wa siasa za kibeberu.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiondoka Chad baada ya kufukuzwa

 

Ufaransa sasa imefukuzwa kutoka katika zaidi ya 70% ya nchi za Kiafrika ambazo ilikuwa na wanajeshi huko. Mkoloni huyu mkubwa wa Ulaya ana uwepo wa kijeshi tu huko Djibouti akiwa na wanajeshi 1500 na huko Gabon ambako ina wanajeshi 350.

Matukio haya yanachukuliwa kuwa sehemu ya mabadiliko mapana ya kimuundo katika ushirikiano wa makoloni ya zamani ya Ufaransa ya Kiafrika katikati ya kuongezeka kwa hisia dhidi ya Wafaransa katika eneo hilo. Viongozi wa Mali, Niger na Burkina Faso wameanzisha uhusiano wa karibu zaidi na Russia na China baada ya kutimuliwa kwa wanajeshi wa Ufaransa. Nchi za Kiafrika zimejikomboa kutoka kwenye pingu za Paris na kuanza kupata taswira huru zaidi.

Wakati wa safari yake katika nchi za Afrika, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisisitiza mara kwa mara kwamba Paris sio adui yenu. Lakini ili kurejesha sura yake katika makoloni yake ya zamani, Ufaransa imekuwa ikifikiria kurejesha sura yake iliyochukiwa na ya kikoloni miongoni mwa vijana wa Kiafrika. Vijana ambao kutokana na kuibuka mlipuko wa taarifa na kuenea kwa njia za mawasiliano wanafuatilia suala la nchi zao kuwa na nafasi katika uga wa kimataifa.

Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana sauti huru zaidi kutoka Afrika inaweza kusikika katika uwanja wa dunia na mbele ya vitovu vingi vya migogoro ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye nchi yake imepata pigo kubwa katika miaka ya hivi karibuni baada ya wanajeshi wake wengi kutimuliwa barani Afrika

 

Hapo awali, Ufaransa ilikuwa inajaribu kuwa na nafasi muhimu katika matukio na maamuzi ya kisiasa ya nchi hizi kwa kuunda Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa (Francophone).  Ufaransa ilikoloni nchi ishirini za Kiafrika kwa miongo kadhaa. Ingawa Ufaransa inajiona kuwa chimbuko la demokrasia, lakini ilifanya njama za kudumisha satwa yake ya kijeshi na kiuchumi barani Afrika kwa kuunga mkono serikali za kidikitea ambazo ni makoloni yake ya zamani.

Baada ya utulivu wa serikali barani Afrika, serikali za Afrika zikiwa katika njia ya matukio ya kimataifa zimechukua mkondo wa ukuaji na maendeleo na zinafuatilia kutumia fursa za kiwango cha juu zaidi kwa ajili ya ustawi na maendeleo. Mataifa ya Afrika hayataki tena kufuata njia ya wakoloni wa zamani ya Ulaya katika uhusiano wao na ulimwengu. Serikali za Kiafrika zinafuatilia uhusiano wenye uwiano na nchi zote za dunia.