Juhudi za uokoaji zinaendelea Ethiopia baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi
Zeozi la kuwahamisha watu linaendelea huko Abomsa katikati mwa Ethiopia kufautia tetemeko la ardhi lililokuwa na ukubwa wa 5.8 kwa kipimo cha rishta kulikumba eneo hilo.
Idara ya kushughulikia maafa na majanga ya kimaumbile ya Ethiopia imesema kuwa imetuma timu ya ufuatiliaji katika wilaya 12 karibu na eneo la tukio ambalo ni makazi ya watu 80,000.
Katika wiki za karibuni, mitetemeko midogo ya ardhi imetokea katika mikoa ya kati na kaskazini mashariki mwa Ethiopia ikiwa ni pamoja na mkoa wa Awash Fentale.
Hali imezidi kuwa mbaya kutokana na mlipuko wa volkano katika Mlima Dofan, ulioko katika eneo panapojiri mara kwa mara mitetemo.
Mitetemeko ya ardhi iliyotokea katika mkoa wa Awash Fentale na maeneo jirani umbali wa kilomita 230 kutoka mji mkuu Addis Ababa iliibua wasiwasi maafa makubwa.