OPEC: Mchango wa nishati ya Libya ni muhimu kwa masoko ya kimataifa
(last modified Mon, 20 Jan 2025 11:10:44 GMT )
Jan 20, 2025 11:10 UTC
  • Haitham al Ghais
    Haitham al Ghais

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Nje Mafuta kwa Wingi (OPEC) amezungumzia nafasi muhimu ya Libya katika soko la nishati duniani, na kusisitiza kuwa maendeleo nchini humo yana mfungamano muhimu na sekta ya kimataifa ya mafuta.

Haitham al Ghais amesisitiza katika Mkutano wa Nishati na Uchumi Libya 2025 huko Tripoli kuwa Libya mejipanga vyema kuwa na nafasi kuu katika sekta ya mafuta na gesi na nishati jadidika.

"Sina shaka kuwa Libya inaweza kuwa mstari wa mbele katika uzalishaji wa mafuta na gesi siku zijazo," amesema Katibu Mkuu wa OPEC.

Haitham al Ghais ameongeza kuwa, Libya ina maliasili mbalimbali kama tulivyoshuhudia na zaidi ya yote serikali ya nchi hiyo imekusudia kuwaletea maendeleo watu wa nchi hiyo.  

Katibu Mkuu wa OPEC amesema Libya imekuwa mwanachama muhimu wa jumuiya hiyo tangu ilipojiunga mnamo 1962. Pia ameeleza kuwa Libya ina akiba kubwa ya mafuta inayokadiriwa kuwa mapipa bilioni 48 (takriban mita za ujazo bilioni 7.6).