Maharamia wa Kisomali waachilia huru meli baada ya siku kadhaa za kuiteka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i124252-maharamia_wa_kisomali_waachilia_huru_meli_baada_ya_siku_kadhaa_za_kuiteka
Maharamia wa Kisomali wameachilia huru meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Yemen ambayo waliiteka nyara tarehe 16 mwezi huu wa Machi katika pwani ya Somalia.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 23, 2025 03:00 UTC
  • Maharamia wa Kisomali waachilia huru meli baada ya siku kadhaa za kuiteka

Maharamia wa Kisomali wameachilia huru meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Yemen ambayo waliiteka nyara tarehe 16 mwezi huu wa Machi katika pwani ya Somalia.

Taarifa zinasema kuwa, meli hiyo, yenye jina la Al-Hidaya na ambayo ilitekwa nyara kwenye eneo la Durdura karibu na Eyl kwenye pwani ya kaskazini mwa Somalia, imetelekezwa na maharamia hao katika eneo la Dhinowda, la kusini mwa eneo ilipokuwa imetekwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wafanyakazi wanane wa Somalia wa meli hiyo walikuwa salama. Hili ni tukio la tatu la uharamia linalohusisha meli ya uvuvi ya Yemen.

Maharamia wa Somalia wameanzisha mashambulizi mbali na fukwe za nchi hiyo.

Kuibuka upya vitendo vya uharamia kumeathiri sekta ya usafirishaji, hivyo kuongeza gharama za bima huku tayari wasafirishaji wakichukua bima ya ziada kwa hatari ya vita, utekaji nyara na fidia, mbali na bima ya kawaida kwa kila shehena.