Wapinzani CAR waandamana kupinga muhula wa tatu wa Rais Touadéra
Maelfu ya waandamanaji wamemiminika katika mitaa ya Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiandamana bega kwa bega na wabunge wa upinzani kupinga vikali taarifa kwamba Rais Faustin-Archange Touadéra wa nchi hiyo anafanya juhudi za kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
Waandamanaji hao karibu 5,000 waliokuwa kwenye safu zilizojaa, huku wakiwa wameshikana mikono na kuimba wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, walipaza sauti zao na kupinga kusalia mamlakani Rais Touadera kwa muhula wa tatu.
Katika mji mkuu Bangui waandamanaji walipiga nara " Zuia muhula wa tatu wa urais", na kisha kuelekea katika mnara wa Boganda ambapo walilakiwa na viongozi wa upinzani.
Viongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameyataja maaandamano hayo kuwa ishara ya wazi ya kushtadi upinzani wa umma. Maandamano ya upinzani katikamji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui yamehudhuriwa pakubwa na kizazi za vijana.
Martin Ziguélé, Mkuu wa chama cha MLPC na shakhsia wa ngazi ya juu wa kambi ya upinzani ya BRDC amesifu harakati hiyo iliyoongozwa na vijana.
Ziguélé amebainisha kuwa: Hivi sasa ambapo Rais Faustin-Archange Touadéra anakaribia kumaliza muhula wake wa pili, anachezea fedha za umma huku akidai kwamba wananchi wanataka aendelee kuiongoza nchi kwa muhula wa tatu". " Asilimia tisini ya walioandamana mjini Bangui ni vijana wa kiume na wa kike.