Watekaji nyara nchini Nigeria wamewaua mateka 35 licha ya kupokea mlungura
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128922-watekaji_nyara_nchini_nigeria_wamewaua_mateka_35_licha_ya_kupokea_mlungura
Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa, maafa mengine yamejiri kaskazini magharibi mwa nchi hiyo baada ya majambazi katika Jimbo la Zamfara kuwaua watu 33 waliowateka nyara mwezi Februari mwaka huu licha ya kupokea pesa ya kikomboleo au mlungura wa zaidi ya dola 33,000.
(last modified 2025-07-29T23:43:47+00:00 )
Jul 29, 2025 23:43 UTC
  • Watekaji nyara nchini Nigeria wamewaua mateka 35 licha ya kupokea mlungura

Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa, maafa mengine yamejiri kaskazini magharibi mwa nchi hiyo baada ya majambazi katika Jimbo la Zamfara kuwaua watu 33 waliowateka nyara mwezi Februari mwaka huu licha ya kupokea pesa ya kikomboleo au mlungura wa zaidi ya dola 33,000.

Raia waliouawa na majambazi ni miongoni mwa wanavijiji 51 waliokuwa wametekwa nyara katika kijiji cha Banga wilayani Kaura Namoda mwezi Februari mwaka huu katika shambulizi la kuvizia lililopelekea kuuliwa watu wawili. 

Baada ya miezi kadhaa ya uchungu na huzuni wa kuwa mbali na ndugu zao, familia za mateka zililipa fedha ya kikomboleo kwa awamu mbili zikitumai kwamba wapendwa wao wataachiwa huru na watekaji nyara.  

Hata hivyo ni mateka 18 tu ambao Ijumaa iliyopita walirejea makwao. Mateka walioachiliwa huru walifichua kuwa, wenzao 33 waliuliwa na majambazi watekaji nyara.

"Walichukua pesa zetu na kuwauwa mateka waliosali," alisikika mkazi mmoja wa jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria. 

Eneo la kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa muda mrefu limeathiriwa na magenge ya watu wanaobeba silaha kali ambao hutekeleza mashambulizi ya kuvizia na jinai mbalimbali dhidi ya raia.