Njaa yaongezeka katika mji wa al Fashir, Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129154-njaa_yaongezeka_katika_mji_wa_al_fashir_sudan
Mamia ya maelfu ya watu waliozingirwa na jeshi la Sudan katika mji wa al Fashir katika jimbo la Darfur wanaishiwa na chakula huku wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya droni na makombora.
(last modified 2025-08-05T02:43:52+00:00 )
Aug 05, 2025 02:43 UTC
  • Njaa yaongezeka katika mji wa al Fashir, Sudan

Mamia ya maelfu ya watu waliozingirwa na jeshi la Sudan katika mji wa al Fashir katika jimbo la Darfur wanaishiwa na chakula huku wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya droni na makombora.

Al Fashir ambayo ni makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini ni uwanja wa vita mkubwa zaidi uliosalia katika jimbo hilo kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha msaada wa haraka (RSF). 

Mamia ya maelfu ya watu waliozingirwa katika jimbo hilo mbali na kuishiwa na chakula wanakabiliwa na hatari ya ugonjwa wa kipindupindu na mashambulizi ya utumiaji mabavu. 

Kuanguka mji huo kungekipa kikosi cha  RSF udhibiti wa karibu Darfur yote; eneo kubwa linalopakana na Libya, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini. 

Daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu ya usalama wake amesema kuwa ukosefu wa chakula ni tatizo kubwa zaidi kuliko mashambulizi. 

" Watoto katika mji wa al Fashir wana utapiamlo, sawa kabisa na watu wazima. Wanamgambo wa kikosi cha msaada wa haraka wamezuia usambazaji wa bidhaa za chakula huku misafara ya misaada ya kibinadamu inayojaribu kufika katika mji huo ikishambuliwa. Wakati huo huo, bei za bidhaa za mahitaji ambazo wafanya magendo wanajaribu kuziiingiza ni mara tano ya wastani wa bei ya kawaida.