Watu 13 wameuawa na 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya RSF Darfur Kaskazini
Mtandao wa Madaktari nchini Sudan leo Jumatatu umetangaza kuwa raia wasiopungua 13 wameuawa na 19 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur Kaskazini.
Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa majeruhi ni pamoja na watoto saba na mama mjamzito. Raia hao wamejeruhiwa katika shambulio lililolenga makazi ya raia khuko al Fasher makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini. magharibi mwa Sudan
Kundi hilo la madaktari limeeleza kuwa raia wengine kadhaa walikuwa wamenasa chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa kufuatia hujuma hiyo ya wanamgambo wa RSF.
Mtandao wa Madaktari wa Sudan umelaani mashambulizi ya kikosi cha RSF na kuyataja kuwa ni jinai kamili za kivita zinazolenga maisha ya raia wa kawada huku jamii ya kimataifa ikinyamaza kimya bila ya kuchukua hatua zozote za kuwalinda mamia ya maelfu ya raia waliokwama huko al Fasher.
Wanamgmbo wa RSF wamewekak mzingiro katika mji wa al Fasher tangiu Mei 10 mwaka jana licha ya indhari za kimataifa kuhusu hatari zinazoweza kusababishwa katika mji huo kufuatia kuzingirwa mji huo ambao ni kitovu cha oparesheni za kibinadamu katika mikoa mitano ya Darfur.
Watu zaidi ya 20,000 wameuawa na wengine milioni 15 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia mapigano ya ndani huko Sudan yaliyoanza katikati ya Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa kikosi cha RSF.