Jeshi la Benin lauwa magaidi 45 kaskazini mwa nchi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135202-jeshi_la_benin_lauwa_magaidi_45_kaskazini_mwa_nchi
Jeshi la Benin limetangaza kuwa limeuwa magaidi 45 katika muda wa miezi mitatu ya oparesheni dhidi ya ugaidi kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-01-07T04:14:51+00:00 )
Jan 07, 2026 04:14 UTC
  • Makamanda wa jeshi, Benin
    Makamanda wa jeshi, Benin

Jeshi la Benin limetangaza kuwa limeuwa magaidi 45 katika muda wa miezi mitatu ya oparesheni dhidi ya ugaidi kaskazini mwa nchi hiyo.

Makundi ya kigaidi yenye mfungamano na mtandao wa al Qaida mara kwa mara yamekuwa yakieneza vitisho vya usalama kaskazini mwa Benin. 

Mwaka 2022, Benin ilituma karibu wanajeshi 3,000 kwa ajili ya kutekeleza oparesheni "Mirador" dhidi ya wanagambo wanaobeba silaha; na tangu wakati huo imeajiri wanajeshi wengine 5,000 ili kuimarisha hali ya usalama kaskazini mwa nchi hiyo.

Kati ya Oktoba na Desemba 2025, jeshi la Benin liliwanasa magaidi 45 na kuwatia nguvuni washukiwa 7, ambao walikabidhiwa kwa mamlaka husika ya mahakama.

Silaha, pikipiki, makopo ya petroli na nk vilikamatwa "wakati wa makabiliano makubwa na adui", imeeleza taarifa ya jeshi la Benin.

Limesema mashinikizo mtawalia yameyazuia makundi yanayobeba silaha kuanzisha makazi ya kudumu katika maeneo ya mipakani.