Mkuu wa Baraza la Utawala Sudan: RSF itaangamizwa hivi karibuni
-
Abdul Fattah al Burhan
Kiongozi wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan amesema kuwa kundi la wapiganaji la Rapid Support Forces (RSF) litaangamizwa hivi karibuni.
Abdul Fattah al Burhan ameiambia televisheni ya al Jazeera ya Qatar kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye hakupatwa na madhara ya kundi la RSF nchini Sudan.
Wakati huo huo jeshi la taifa la Sudan limetangaza kuwa limefanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya ngome za RSF katika maeneo ya Darfur na Kordofan.
Taarifa hiyo imesema, magari 240 ya wapiganaji wa RSF yameharibiwa katika hujuma hiyo kubwa na kwamba ndege zisizo na rubani za kistatijia za kundi hilo pia zimehariibiwa katika uwanja wa ndege wa Niala.
Jeshi la Sudan limesema, sasa wapiganaji wa RSF wamefukuzwa katika eneo kubwa la jimbo la Kordofan.
Mapigano kati ya jeshi la taifa la Sudan na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika miji ya Kordofan tangu wapiganaji wa RSF walipoimarisha uwepo wao katika eneo lote jirani la Darfur, na kudhibiti mji wa El Fasher mwezi Oktoba mwaka uliopita.