Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135324-umoja_wa_mataifa_watu_milioni_30_nchini_sudan_wanahitajia_msaada_wa_haraka
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu.
(last modified 2026-01-10T08:39:48+00:00 )
Jan 10, 2026 08:39 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka
    Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, vita na mzozo katika nchi ya Sudan umeingia katika siku yake ya 1,000, na zaidi ya Wasudan milioni 30 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema: raia wanapitia vurugu mbaya na kulazimishwa kuhama, wakiishi katika hali mbaya. Wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na dawa, na wanakabiliwa na magonjwa mengi.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo inasema: Misaada ya kibinadamu kwa kiasi kikubwa haitoshi kutokana na ugumu wa upatikanaji.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema, kukosekana kwa matarajio yoyote ya suluhisho la kisiasa na uzito wa hali hiyo kunatokana na ukubwa wa vurugu kama vile ukosefu wa msaada mkubwa wa kimataifa.

Jeshi la Sudan bado linasisitiza kwamba litaendelea na vita hadi litakapoondoa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). RSF inatawala kabisa Darfur na sehemu muhimu za Kordofan kusini na magharibi mwa nchi. Jeshi kwa sasa linaendelea kusonga mbele Kordofan.

Kundi la madakatri wa Sudan limetahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kiafya na kibinadamu katika mji wa Dalang unaopatikana katika jimbo la Kordofan Kusini. Kundi hilo limesema kuwa mji wa Dalang unaendelea kuzingirwa huku ukikabiliwa na mashambulizi makali ya wanagambo wa RFS.

Sudan ilitumbulia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 15,  2023 kufuaatia uchu wa madaraka kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Abdel Fattah al-Barhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo.