Ghana imelipa deni la dola bilioni 1.47 la sekta ya nishati
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135422-ghana_imelipa_deni_la_dola_bilioni_1.47_la_sekta_ya_nishati
Ghana imelipa jumla ya dola za Marekani bilioni 1.47 mwaka 2025 ili kufuta madeni ya muda mrefu ya sekta ya nishati na kurejesha dhamana ya Benki ya Dunia kwa sekta hiyo. HIi ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Wizara ya Fedha ya nchi hiyo.
(last modified 2026-01-13T00:13:45+00:00 )
Jan 13, 2026 00:13 UTC
  • Cassiel Ato Forson Waziri wa Fedha wa Ghana
    Cassiel Ato Forson Waziri wa Fedha wa Ghana

Ghana imelipa jumla ya dola za Marekani bilioni 1.47 mwaka 2025 ili kufuta madeni ya muda mrefu ya sekta ya nishati na kurejesha dhamana ya Benki ya Dunia kwa sekta hiyo. HIi ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Wizara ya Fedha ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Cassiel Ato Forson Waziri wa Fedha wa Ghana, serikali ya nchi hiyo imelipa kikamilifu dola za Kimarekani milioni 597.15, ikiwa ni pamoja na riba, iliyotolewa kama sehemu ya Dhamana ya Hatari ya Benki ya Dunia.

Ulipaji huo wa madeni umerejesha dhamana ambayo ni muhimu katika kurejesha imani ya wawekezaji katika sekta ya nishati ya Ghana.

Waziri Forson ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa X unaosomeka: Sekta ya nishati iliyumba wakati Rais John Dramani Mahama wa Ghana alipoingia madarakani Januari mwaka jana kufuatia miaka kadhaa ya kutolipwa gesi inayotolewa kwa sekta ya nishati ya nchi hiyo. 

Amesema: Wakati Rais Mahama alipoanza kazi Januari mwaka jana sekta ya nishati ilikuwa imesukumwa ukingoni baada ya miaka mingi ya kutolipa kwa gesi inayotolewa kwa sekta hiyo. 

Waziri wa Fedha wa Ghana amesema kuwa serikali inauhakikishia umma kwa ujumla, wadau wa sekta hiyo na washirika wa kimataifa kwamba enzi ya ulimbikizaji wa madeni ya sekta ya nishati isiyodhibitiwa imekwisha.

MBali na kulipa deni hilo, serikali ya Ghana pia imelipa takriban dola za  milioni 393 katika madeni iliyokuwa ikidaiwa na wazalishaji binafsi wa umeme (IPPs), na hivyo kuleta utulivu katika sekta hiyo.