Katibu mkuu wa kamati ya olimpiki nchini Kenya atiwa mbaroni kwa ufisadi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14045-katibu_mkuu_wa_kamati_ya_olimpiki_nchini_kenya_atiwa_mbaroni_kwa_ufisadi
Duru za usalama nchini Kenya zimeripoti kutiwa mbaroni Katibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2016 02:56 UTC
  • Katibu mkuu wa kamati ya olimpiki nchini Kenya atiwa mbaroni kwa ufisadi

Duru za usalama nchini Kenya zimeripoti kutiwa mbaroni Katibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki nchini humo.

Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema kuwa, Francis K. Paul ametiwa mbaroni kufuatia pendekezo la serikali ya nchi hiyo baada ya kutuhumiwa kuhusika na ufisadi wa kifedha na makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni huko mjini Rio De Janeiro nchini Brazil.

Wanariadha wa Kenya wakiwa katika mashindano ya mbio

Habari zaidi zimeeleza kwamba viongozi wa serikali wanaendelea na uchunguzi dhidi ya viongozi wengine wa  Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya nchi hiyo. Duru ya 31 ya michezo ya olimpiki mwaka 2016 ilianza mnamo tarehe 6 hadi 21 mwezi huu huko mjini Rio De Janeiro nchini Brazil.