Sep 05, 2016 14:12 UTC
  • Maandamano dhidi ya Zuma mbele ya makao makuu ya ANC

Wanachama wa chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) leo Jumatatu wamepiga nara na shaari nje ya makao makuu ya chama hicho wakimtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu.

Wafuasi hao wa chama cha ANC wamejitokeza leo mbele ya makao makuu ya chama hicho huko Johannesburg wakitaka kujiuzulu Zuma katika hatua ambayo imetajwa kuwa ya nadra kushuhudiwa kufanywa na wanachama wa ANC baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi wa mabaraza ya miji tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini mwaka 1994.

Maandamano dhidi ya Zuma nje ya makao makuu ya ANC huko Johannesburg

Wafanya maandamano wamesema kuwa Zuma ambaye uongozi wake umekumbwa na kashfa anapaswa kulaumiwa kwa kushindwa chama tawala katika uchaguzi wa mabaraza ya miji kwenye miji mikubwa mitatu mwezi uliopita, kulikosababishwa na usimamiaji mbaya wa uchumi wa  nchi ambao sasa unakaribia kusambaratika. Waaandamanaji hao wa ANC ambao walikuwa chini ya mia moja walibeba mabango yanayosomeka "Jiuzulu mara moja Kamati Kuu ya ANC na Jacob Zuma.''

 

 

 

 

 

 

Tags