Sep 07, 2016 07:51 UTC
  • HRW: Wapiganaji wa Niger Delta wasisamehewe kwa jinai zao

Taasisi moja ya kutetea haki za binaadamu nchini Nigeria imetaka kutosamehewa na rais wapiganaji wa kundi la ulipizaji kisasi la Niger Delta nchini humo.

Hayo yamesemwa na Torkuma Venatius, mkuu wa taasisi ya kutetea haki za binaadamu nchini Nigeria na kubainisha kwamba, wapiganaji wa kundi hilo ni magaidi ambao wanatakiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma dhidi yao. Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo kutaka kutoa msamaha kwa wanachama wa genge hilo. Torkuma Venatius amesisitiza kuwa, kundi la ulipizaji kisasi limehusika katika hujuma dhidi ya taasisi za mafuta na gesi nchini humo ambazo zinahesabiwa kuwa vyanzo vya kitaifa.

Picha ya Rais Buhari wa Nigeria, na waasi wa Niger Delta

Kwa mara kadhaa sasa wanachama wa kundi hilo la ulipizaji kisasi la Niger Delta wamekuwa wakishambulia taasisi za mafuta katika eneo hilo kwa lengo la kuitia hasara serikali ya Rais Buhari ambaye wanamtuhumu kwa kutozingatia maslahi ya wananchi. Hujuma hizo zimepelekea kupungua kiwango cha uzalishaji mafuta nchini Nigeria kutoka mapipa milioni mbili kwa siku na kufikia milioni moja na nusu.

Tags