Oct 04, 2019 01:39 UTC
  • Afrika Kusini na Nigeria zaboresha uhusiano na kufikia makubaliano ya kibiashara

Afrika kusini na Nigeria jana Alhamisi zilisaini hati 30 za makubaliano ya ushirikiano, wiki kadhaa baada ya wimbi la ghasia na machafuko yaliyowalenga raia wa nchi za Afrika katika miji ya Johannesburg na Pretoria. Machafuko hayo yalivuruga uhusiano kati ya nchi mbili hizo za Afrika zenye uchumi mkubwa.

Mwezi Septemba mwaka huu kundi la watu waliokuwa na silaha walivamia biashara na makazi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini na kuua watu kumi na kujeruhi makumi ya wengine. Watu wasiopungua 400 walitiwa mbaroni kwa kuhusika na mashambulizi hayo.

Baada ya mashambulizi hayo, Nigeria iliwarudisha nyumbani raia 600 waliokuwa wakiishi Afrika Kusini ili kuepa mashambulizi dhidi ya raia wageni wa nchi za Kiafrika.  

Mashambulizi dhidi ya raia wageni wa Kiafrika nchini Afrika Kusini

 

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari wamesema mwishoni mwa ziara ya Rais Buhari mjini Pretoria kwamba, wanasikitishwa na mchafauko na vitendo vya ulipizaji kisasi dhidi ya biashara za raia wa Afrika Kusini huko Nigeria na badala yake wameahidi kuboresha zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili hizo.

Rais wa Afrika Kusini amesema kuwa, katika mkutano wake wa jana na Rais wa Nigeria pande hizo mbili zumesaini makubaliano 32 katika sekta za viwanda na biashara, na sayansi na teknolojia, ulinzi, kilimo na nishati.  

Tags