Oct 07, 2024 11:03 UTC
  • Wanachuoni 3,000 wa Kisuni wamwandikia barua ya shukrani Kiongozi Muadhamu

Wanachuoni 3,000 wa Kisuni wa nchini Iran wamemwandikia barua ya shukrani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wakimshukuru na kumpongeza kwa operesheni ya Ahadi ya Kweli II iliyoutia adabu utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, katika barua yao hiyo kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, maelfu ya wanachuoni hao wa Kisuni wa nchini Iran wamesema: "Hivi sasa baada kutokana na uongozi wako wa busara na uliojaa hekima na baada ya kupita muda wa kujizuia kifakhari, hatimaye jeshi lenye nguvu la SEPAH la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran limeyapiga kwa makombora maeneo ya ndani kabisa ya utawala wa Kizayuni na kuzitia furaha nyoyo zilizokuwa zimejaa majonzi za mashahidi na wananchi wasio na ulinzi wa Palestina na nyoyo za wapenda haki wote duniani. 

Sisi (wanachuoni 3,000 wa Kisuni) ambao tunajumuisha Maimamu wa Ijumaa na Sala za Jamaa na wafanya tablighi wa Kisuni nchini (Iran), tukiwa ni watumikiaji wa Qur'ani na mafundisho ya Kiislamu katika njia ya mshikamano na "Jihadi ya Upambanuzi" na kubainisha ukweli wa mambo, sambamba na kukushukuru kwa miongozo yako ya busara sana uliyoitoa kwenye khutba za Sala ya Ijumaa zilizomtikisa adui, tunakushukuru sana kwa dhati ya moyo kutokana na operesheni ya "Ahadi ya Kweli II" iliyofanywa kishujaa na vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala ghasimu unaoua kwa umati watoto wadogo wa Palestina.