Araghchi akosoa uzembe wa Baraza la Usalama katika kukabiliana na jinai za Israel
(last modified Sun, 06 Oct 2024 02:51:35 GMT )
Oct 06, 2024 02:51 UTC
  • Araghchi akosoa uzembe wa Baraza la Usalama katika kukabiliana na jinai za Israel

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa uzembe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na vitendo haramu na jinai za utawala wa Kizayuni ambazo zinafanyika kwa himaya na uungaji mkono wa Marekani na Uingereza.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo mjini DaMascus Syria katika mazunguumzo yake na Bassam al-Sabbagh, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo ambapo wawili hao wamejadili pia masuala ya pande mbili, kieneo na kimataifa.

Katika mkutano huo, pande hizo zilipitia na kubadilisha mawazo kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika uhusiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kiusalama, na kujadili njia za kuimarisha ushirikiano na kutekeleza kikamilifu makubaliano na hati za ushirikiano zilizotiwa saini kati ya nchi hizo mbili.

Sambamba na kukosoa uungaji mkono wa Marekani na Uingereza kwa utawala wa Kizayuni na kukwamisha kwao uamuzi wowote wa maana wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, taarifa ya pamoja ya hivi karibuni ya nchi 10 zisizo wanachama wa baraza hilo ya kutaka kusimamishwa mara moja hujuma za kijeshi za utawala wa Kizayuni kuwa ni hatua  muhimu.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alielekea Syria hapo jana akitokea Lebanon ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo.

Tags