Ethiopia yaachilia huru mamia ya wafungwa wakiwemo Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15166-ethiopia_yaachilia_huru_mamia_ya_wafungwa_wakiwemo_waislamu
Ethiopia imetangaza kuwaachilia huru mamia ya wafungwa wakiwemo Waislamu ambao walikuwa wanashikiliwa kwa kupinga uingiliaji wa serikali katika mambo yao ya kidini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2016 03:34 UTC
  • Ethiopia yaachilia huru mamia ya wafungwa wakiwemo Waislamu

Ethiopia imetangaza kuwaachilia huru mamia ya wafungwa wakiwemo Waislamu ambao walikuwa wanashikiliwa kwa kupinga uingiliaji wa serikali katika mambo yao ya kidini.

Mwendesha Mashtaka Mkuu Getachew, amesema karibu watu 1,000 wameachiliwa huru kwa minasaba ya mwaka mpya wa Kiethiopia na Siku Kuu ya Idul Adha. Amesema kati ya wafungwa hao kulikuwa na Waislamu 135 ambao walikuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za ugaidi kutokana na misimamo yao ya kuandamana kutetea haki zao.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2012, Ethiopia iliwafunga vifungo virefu gerezani Waislamu ambao walishiriki katika maandamano ya miezi kadhaa kupinga hatua ya serikali kukiuka katiba kwa kuunga mkono kundi la Kisufi la Al Ahbash na kuwalazimisha Waislamu kufuata kundi hilo.

Kati ya walioachiliwa huru ni Yusuf Getachew, Mhariri mkuu wa Jarida la Ye Muslimoch Guday (Masuala ya Waislamu) ambaye amekuwa akishikiliwa kizuizini tokea Julai 2012.

Maandamano dhidi ya serikali Ethiopia

 

Aidha katika miezi ya hivi karibuni, Ethiopia imekuwa ikishuhudia maandamano ya makabila ya Oromo na Amhara ambayo yanalalamikia siasa mbovu za serikali ya Addis Ababa. Makabila hayo mawili yanaikosoa serikali kuu kwa kufanya ubaguzi kwa maslahi ya watu wa kabila la Tigré.