Sep 21, 2016 07:12 UTC
  • Machafuko yashtadi eneo la Niger Delta huko nchini Nigeria

Hali ya wasi wasi na machafuko vimeshtadi katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta, kusini mwa Nigeria kutokana na kundi la ulipizaji kisasi la Niger Delta kuongeza hujuma zake za kushtukiza.

Kwa mujibu wa duru za habari nchini Nigeria, wanachama wa kundi hilo la ulipizaji kisasi la Niger Delta, wametoa ripoti wakitangaza kuhusika kwao katika hujuma dhidi ya bomba la mafuta la Shirika la Mafuta la nchi hiyo lililotokea hivi karibuni katika eneo hilo. Hii ni katika hali ambayo mashambulizi ya wabeba silaha na ukatili vimewatia wasi wasi mwingi wakazi wa eneo hilo huku watu 23 wakiripotiwa pia kuuawa.

Moto ukiyateketeza mabomba ya mafuta eneo hilo

Sanjari na hali hiyo jeshi la Nigeria limetangaza azma yake ya kukabiliana na waasi wa eneo hilo katika kujaribu kurejesha hali ya usalama na uthabiti. Kwa mujibu wa jeshi hilo, katika operesheni zilizopewa jina la 'Tabasamu la Mambo' askari wa serikali wamefanikiwa kuangamiza vituo 74 vya kuzalisha na kuuza mafuta ya magendo vilivyokuwa vinamilikiwa na waasi, sanjari na kudhibiti kiwango kikubwa cha silaha na zana za kijeshi. Waasi wa eneo hilo la Niger Delta wanamtuhumu Rais Muhammadu Buhari kwa kutojali maslahi ya wananchi wa nchi hiyo.

Tags