Mjumbe wa UN asisitiza kufanyika mazungumzo kuhusu mgogoro wa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19480-mjumbe_wa_un_asisitiza_kufanyika_mazungumzo_kuhusu_mgogoro_wa_libya
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Libya amesema kuwa mazungumzo na kujiepusha na mivutano ya kijeshi huko Libya ndiyo njia pekee itakayoupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2016 23:22 UTC
  • Mjumbe wa UN asisitiza kufanyika mazungumzo kuhusu mgogoro wa Libya

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Libya amesema kuwa mazungumzo na kujiepusha na mivutano ya kijeshi huko Libya ndiyo njia pekee itakayoupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Martin Kobler ameyasema hayo mjini Cairo katika mazungumzo yake na Muhammad al Kashki Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, na amezitaka pande hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Libya.

Martin Kobler Mjumbe Maalumu wa UN nchini Libya

Libya ilitumbukia katika migawanyiko ya kisiasa na hatimaye kuanzishwa serikali mbili, moja ikiwa na makao Tripoli magharibi mwa Libya na nyingine huko Tobruk mashariki mwa nchi, baada ya kupinduliwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Mwezi Machi mwaka huu kuliaundwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa nchini Morocco lakini hadi sasa serikali hiyo inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa haijafanikiwa kudhibiti ardhi yote ya nchi hiyo.