Sudan Kusini ipo tayari kutumwa kikosi kipya cha UN nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20257-sudan_kusini_ipo_tayari_kutumwa_kikosi_kipya_cha_un_nchini_humo
Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa ipo tayari kuafiki kutumwa nchini humo kikosi kipya cha kudumisha amani wakati wowote, baada ya mapigano ya mwezi Julai huko Juba kutishia kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vikubwa.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Nov 27, 2016 01:16 UTC
  • Sudan Kusini ipo tayari kutumwa kikosi kipya cha UN nchini humo

Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa ipo tayari kuafiki kutumwa nchini humo kikosi kipya cha kudumisha amani wakati wowote, baada ya mapigano ya mwezi Julai huko Juba kutishia kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vikubwa.

Sudan Kusini imekuwa chini ya mashinikizo ya kimataifa ikitakiwa ikubali kutumwa kikosi cha wanajeshi wa UN kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama ambacho kitakisaidia kile cha UNMISS. Akol Paul Kordit Naibu Waziri wa Habari wa Sudan Kusini amesema kuwa serikali imeafiki masuala yaliyokuwa hayajatatuliwa katika kikao chake cha juzi, ingawa naibu huyo waziri hakutaja ni masuala yapi.

Kikosi cha kudumisha amani cha UN kilichopo Sudan Kusini (UNIMISS)

Mtaalamu mmoja ambaye amekuwa akifuatilia mchakato huo amebainisha kuwa masuala yaliyokuwa hayajapatiwa ufumbuzi yalikuwa ni kuhusu nchi wanakotoka walinda amani hao, aina ya silaha na idadi sahihi ya wanajeshi katika kikosi hicho kipya ambacho kitakiimarisha kile cha Umoja wa mataifa kilichopo Sudan Kusini UNMISS.