Wahajiri wanne waaga dunia katika Bahari ya Kati (Mediterranean)
(last modified Wed, 07 Dec 2016 15:45:03 GMT )
Dec 07, 2016 15:45 UTC
  • Wahajiri wanne waaga dunia katika Bahari ya Kati (Mediterranean)

Maafisa husika wa Morocco wameeleza kuwa wahajiri wanne wameaga dunia baada ya kuzama boti yao iliyokuwa imebeba makumi ya wahajiri katika maji ya bahari ya Mediterania kati ya Morocco na Uhispania.

Maafisa wa Uhispania wameeleza kuwa vikosi vya majini, polisi na idara ya uokoaji ya nchi hiyo wameopoa majini miili ya wahajiri walioaga dunia na kuwaokoa wahajiri wengine.

Maafisa wa Morocco pia wameeleza kuwa wahajiri wengine 34 wameokolewa majini katika mji wa al Hasime kaskazini mwa Morroco.  Wahajiri hao wengi wanatoka katika nchi za kusini mwa eneo la Jangwa la Sahara. Miili ya wanawake watano pia inaonekana miongoni mwa wahajiri walioga dunia huko Morocco.

Wahajiri walionusurika kufa maji huko Morocco wakielekea Ulaya 

Tayari uchunguzi umeanzishwa kuhusu wahajiri hao haramu huko Morocco. Maafisa wa Uhispania awali walitangaza kuwa wahajiri 64 wameokolewa  wakiwa katika boti mbili katika maji ya bahari ya Mediterania kati ya Uhispania na Morocco. Shirika la Kimataifa la Wahajiri limetangaza kuwa mwaka 2015 liliwaokoa majini wahajiri karibu 3850 ambao walikuwa wakitaka kuvuka maji ya Mediterania na kuelekea Ulaya. 

Tags