Waislamu wa Nigeria walaani njama za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21160-waislamu_wa_nigeria_walaani_njama_za_israel
Waislamu wa Kishia nchini Nigeria wamelaani njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kukwamisha juhudi za kuachiliwa huru Sheikh Zakzaki, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2016 12:08 UTC
  • Sheikh Ibrahim Zakzaki, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
    Sheikh Ibrahim Zakzaki, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Waislamu wa Kishia nchini Nigeria wamelaani njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kukwamisha juhudi za kuachiliwa huru Sheikh Zakzaki, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kusema kuwa, Waislamu hao wamefanya maandamano nchini Nigeria na sambamba na kushinikiza kutekelezwa haraka amri ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo ya kuachiliwa huru kiongozi wa harakati ya Kiislamu bila ya masharti yoyote wameulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kufanya njama za kuishinikiza serikali ya Nigeria ibatilishe uamuzi huo wa mahakama.

Mahakama Kuu ya Nigeria imetoa amri ya kuachiliwa huru bila ya masharti yoyote Sheikh Zakzaki katika hali ambayo Waislamu wa nchi hiyo wamekuwa wakifanya maandamano ya amani ya mfululizo kwenye maeneo tofauti ya Nigeria kulalamikia marufuku ya kutofanya mikusanyiko yoyote ya kidini na kusisitiza kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba, 

Waislamu wa nchini Nigeria

 

Tarehe 13 Disemba 2015, jeshi la Nigeria lilivamia mji wa Zaria wa kaskazini mwa jimbo la Kaduna wakaua idadi kubwa ya Waislamu na kuwajeruhi wengine wengi. Aidha walimpiga risasi Sheikh Zakzaki na baadaye kumkamata na kumuweka korokoroni kinyume cha sheria.