Umoja wa Ulaya: Makundi ya kisiasa Gabon yafanye mazungumzo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21538-umoja_wa_ulaya_makundi_ya_kisiasa_gabon_yafanye_mazungumzo
Umoja wa Ulaya umeyataka makundi ya kisasa nchini Gabon kufanya mazungumzo mapana kuhusu suala la kutaka kuitisha tena uchaguzi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2016 11:35 UTC
  • Umoja wa Ulaya: Makundi ya kisiasa Gabon yafanye mazungumzo

Umoja wa Ulaya umeyataka makundi ya kisasa nchini Gabon kufanya mazungumzo mapana kuhusu suala la kutaka kuitisha tena uchaguzi nchini humo.

Umoja wa Ulaya umesema leo katika taarifa yake kuwa ujumbe wake uliokutana na Waziri Mkuu wa Gabon umesisitiza kuanza mazungumzo makuu ya kisiasa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na waangalizi wa uchaguzi. Taarifa ya Umoja wa Ulaya imebainisha kuwa, mazungumzo ya kisiasa ya Gabon yanapasa kujumuisha suala la kufanyiwa marekebisho mchakato wa uchaguzi, taasisi na vyombo vya mahakama nchini humo. Serikali ya Gabon pia imetangaza utaarifu wake wa kuanza mazungumzo na Umoja wa Ulaya katka sehemu yoyote inayowezekana.

Ali Bongo aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Rais wa mwaka huu nchini Gabon 

Mazungumzo kati ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya na Waziri Mkuu wa Gabon yamefanyika baada ya waangalizi wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 27 mwaka huu kuwasilisha ripoti yao ya mwisho kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi. Katika ripoti hiyo, Waangalizi hao wa Umoja wa Ulaya wametilia shaka matokeo ya uchaguzi wa rais wa Gabon ambayo yalimtangaza Ali Bongo kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa mara nyingine.

Itakumbukwa kuwa mwanadiplomasia Jean Ping ambaye alikuwa mgombea wa upinzani aliyechuana na Ali Bongo katika kinyang'anyiro hicho alipinga matokeo hayo ya uchaguzi yaliyomtangaza mshindi Ali Bongo.