Kenya yazidisha usalama sherehe za Krismasi na mwaka mpya wa 2017
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22126-kenya_yazidisha_usalama_sherehe_za_krismasi_na_mwaka_mpya_wa_2017
Vyombo vya usalama vya Kenya vimechukua hatua kali za kulinda usalama sambamba na sherehe za Krismasi na mwaka mpya wa 2017 kwa ajili ya kukabiliana na tishio lolote la kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2016 12:27 UTC
  • Kenya yazidisha usalama sherehe za Krismasi na mwaka mpya wa 2017

Vyombo vya usalama vya Kenya vimechukua hatua kali za kulinda usalama sambamba na sherehe za Krismasi na mwaka mpya wa 2017 kwa ajili ya kukabiliana na tishio lolote la kigaidi.

Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema kuwa, hatua hizo kali za usalama zimechukuliwa baada ya mashambulizi kadhaa yaliyofanywa hivi karibuni na kundi la kigaidi la al Shabab katika maeneo ya raia na kwamba askari polisi wamesambazwa katika maeneo mbalimbali ya Kenya kwa ajili ya kufuatilia harakati za wanachama wa kundi hilo hususan maeneo yanayokaribia mpaka wa nchi hiyo na Somalia. 

Polisi wa Kenya katika operesheni ya kusaka al Shabab

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Nkaissery amesema serikali ya Nairobi ina azma kubwa ya kung'oa kikamilifu mzizi wa kundi la kigaidi la al Shabab. Waziri Nkaissery ameongeza kuwa, jeshi la Kenya limezidisha operesheni zake katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Somalia baada ya kuongezeka vitisho vya kundi hilo. 

Jumamosi ya jana magaidi wa kundi la al Shabab walishambulia eneo la Wajiir huko kaskazini mashariki mwa Kenya na kuua raia wawili.