Iran na Zimbabwe zajadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29214-iran_na_zimbabwe_zajadili_njia_za_kuimarisha_ushirikiano_wa_kiuchumi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zimejadili njia mbalimbali za kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi mbili hizo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 17, 2017 13:57 UTC
  • Iran na Zimbabwe zajadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zimejadili njia mbalimbali za kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi mbili hizo.

Hayo yamesisitizwa katika mazungumzo baina ya balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Harare na Waziri wa Viwanda wa nchi hiyo ya Kiafrika.

Katika mazungumzo hayo, Ahmad Erfanian, balozi wa Iran mjini Harare na Mike Bimha Waziri wa Viwanda wa Zimbabwe, wamejadili jinsi ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tehran na Harare.

Ahmad Erfanian amesema katika mazungumzo yake na waziri Bimha kwamba, kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Iran na Zimbabwer hakiridhishi licha ya nchi mbili kuwa na uhusiano mzuri.

Ahmad Erfanian (kulia), balozi wa Iran mjini Harare na Mike Bimha Waziri wa Viwanda wa Zimbabwe

Kadhalika pande mbili hizo zimekubaliana kuongeza kiwango cha mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara baina ya nchi mbili hususan katika nyuga za sayansi, teknolojia, elimu, uchimbaji madini na kilimo.

Kwa upande wake Mike Bimha, Waziri wa Viwanda wa Zimbabwe amesema kuwa, nchi yake inakaribisha kwa mikono miwili kuimarishwa uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.

Wakati huo huo, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo an Spika wa Baraza la Seneti la Zimbabwe ambapo wamesisitiza katika mazungumzo yao juu ya azma ya nchi hizo ya kukuza ushirikiano katika nyanja mbalimbali.