Mripuko wa homa ya ndege waripotiwa Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29852-mripuko_wa_homa_ya_ndege_waripotiwa_kongo_dr
Mripuko wa homa hatari ya ndege imeripotiwa katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2017 10:25 UTC
  • Mripuko wa homa ya ndege waripotiwa Kongo DR

Mripuko wa homa hatari ya ndege imeripotiwa katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Shirika la Afya ya Wanyama Duniani OIE limetangaza leo Jumatano kuwa, homa hiyo ya ndege aina ya H5 imegunduliwa katika vijiji vitatu vilivyoko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Uganda.

Kadhalika Wizara ya Afya ya Kongo DR imethibitisha kutokea mripuko huo, miezi michache baada ya homa hiyo kuripotiwa katika nchi jirani ya Uganda.

Januari mwaka huu, serikali ya Uganda ilitangaza mripuko wa homa ya ndege aina ya H7N9, katika wilaya za katikati mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Wilaya zilizoathiri zaidi na virusi hivyo hatari ni Masaka, Entebbe, baadhi ya maeneo ya mji mkuu Kampala na fukwe za Ziwa Victoria.

Kawaida wanadamu hawaambukizwi homa ya ndege 

Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), homa ya ndege ni ugonjwa unaoambukizwa na ndege kupitia kirusi cha avian ambacho kiada sio chenye kuambukiza mwanadamu lakini imewahi kusababisha matatizo ya kupumua kwa wanadamu.

Nigeria, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Afrika Kusini zimewahi kuripoti mripuko wa homa ya ndege katikati ya mwaka uliopita wa 2016.