Pars Today
Rwanda imeanza kutoa dozi za chanjo ya virusi vya Marburg ili kujaribu kudhibiti mripuko wa ugonjwa huo unaofanana na Ebola katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Idadi ya wagonjwa nchini Uganda walioambukizwa aina mpya ya virusi vya Mpox imeongezeka hadi 11, huku afisa mkuu wa afya akiripoti kuwa hakuna vifo vilivyosababishwa na maradhi hayo kufikia jana Jumamosi nchini humo.
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mripuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu katika jimbo la Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria imeongezeka na kufikia 21.
Zimbabwe imetangaza hali ya dharura katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare, kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambo umeua makumi ya watu, mbali na maelfu ya wengine kupata maambukizi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaka jamii ya kimataifa ishirikiane na kuiunga mkono Tanzania katika kupambana na mripuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema nchi 37 za bara Afrika zinakabiliwa na hatari kutokana na uhaba wa wahudumu wa afya.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa, karibu robo tatu ya nchi wanachama wa taasisi hiyo hazina sera za kupunguza kwa lazima matumizi ya juu ya chumvi.
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu ongezeko la kutisha la kesi za utapiamlo mkali miongoni mwa wanawake wajawazito hususan katika nchi za Afrika.
Viongozi wa sekta za afya Afrika wamesema dunia haitafanikiwa kuwa na usalama wa afya, iwapo nchi za bara hilo zitaendelea kutengwa.
Uganda imetangaza habari ya kudhibitiwa na kutokomezwa mlipuko wa Ebola ambao umeua makumi ya watu nchini humo tangu Septemba mwaka uliomalizika 2022.