Manowari ya Ireland yaokoa wahajiri 712 karibu na Libya
(last modified Mon, 26 Jun 2017 16:08:18 GMT )
Jun 26, 2017 16:08 UTC
  • Manowari ya Ireland yaokoa wahajiri 712 karibu na Libya

Manowari moja ya Ireland imewaokoa watu 712 wakiwemo akinamama wajawazito na watoto wachanga katika pwani ya mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Uokoaji huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya operesheni ya kuwanusuru kufa baharini wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya. Manowari hiyo kwa jina la "The Le Eithne" jana kwa siku nzima iliongoza operesheni ya kuziokoa meli kadha umbali wa kilomita 40 kaskazini magharibi mwa Tripoli.

Wahajiri sita akiwemo mtoto mmoja waliweza kuokolewa kutoka katika meli hizo wakiwa wamepoteza fahamu. Manowari hiyo ya Ireland itawasafirisha wahajiri waliokolewa wakiwemo akinamama wajazizto 14 na watoto wachanga wanne walio na umri chini ya miezi minne hadi katika bandari salama na kisha watakabidhiwa kwa maafisa husika wa Italia.

Manowari ya Ireland katika oparesheni ya kuwaokoa wahajiri haramu 

Kamanda Brian Fitzgerald anayeongoza manowari hiyo amesema kuwa anaona fakhari kueleza kuwa, wamefanikiwa kuokoa maisha ya watu hao wote na kwamba operesheni ya uokoaji ilikuwa ngumu kwa sababu maisha ya watu yalikuwa hatarini.

Tags