Watu tisa wauawa katika shambulizi la kigaidi Maiduguri, Nigeia
Watu waliokuwa wamejifunga mabomu wamejilipua na kuuwa watu wanne na kujeruhi wengine 13 katika milipuko iliyotokea kwa wakati mmoja katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Hayo yameelezwa leo na polisi ya Borno. Wiki kadhaa zilizopita pia makao makuu hayo ya jimbo la Borno na maeneo ya karibu yake yalikumbwa na mashambulizi kadhaa ya kujilipua kwa mabomu ukiwemo mlipuko uliotokea tarehe 19 mwezi huu na kuuwa watu 12 na ule wa Juni 7 uliosababishwa vifo vya watu 14.
Polisi ya Borno imeeleza kuwa, mwanaume mmoja aliyekuwa amejifunga mabomu jana jioni alijilipua na kumuuwa mlinzi mmoja baada ya kuingia katika Chuo Kikuu cha Maiduguri katikati mwa mji huo. Aidha wanawake wanne waliokuwa wamejifunga mabomu waliua watu wanane katika kitongoji cha Zannari nje kidogo ya mji wa Maiduguri, saa mmoja baada ya kutokea mlipuko wa kwanza. Wanawake hao walitenda jinai hiyo katika nyumba za makazi ya raia.
Idara ya Usalama wa Taifa ya Nigeria Ijumaa iliyopita ilitangaza kuwa, imesambaratisha njama za kutaka kulipua mada za milipuko katika miji minne ya kaskazini mwa nchi hiyo yaani Maiduguri, Kano, Sokoto na Kaduna wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Idul Fitr.